SHUGHULI
ZA SHIRIKA LA FLCAD
Shirika linafanya shughuli zinazohusiana na:-
- KILIMO
- UHIFADHI MAZINGIRA
Shirika linatoa elimu juu ya utunzaji wa
Mazingira kwa kutoa mbegu za miti na miche ya miti aina mbali mbali na mafunzo juu ya uanzishaji na utunzaji wa vitalu vya
miche ya miti na upandaji. Pia linatoa elimu ya
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuhimiza kutokuchoma moto ovyo, kutokata
miti ovyo, kupunguza matumizi ya mkaa na
kuni, katika kipengele hiki shirika
linawezesha jamii kutengeneza na kutumia majiko banifu ya mkaa na kuni, Matumizi
ya Nishati mbadala (Solar energy na Biogas), Shirika pia linawezesha jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji.
Pia shirika
limeanzisha vikundi vya Mazingira mashuleni (Environmental school club) katika
mashule watoto wanafundishwa utunzaji wa mazingira, Uanzishaji wa miradi ya
bustani za mboga mboga na matunda, Mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya
kuyakabili
- UFUGAJI
Shirika linatoa
elimu juu ya ufugaji rafiki wa mazingira kwa kuelimisha jamii kufuga mifugo
michache yenye tija, Pia shirika linatoa nguruwe, kuku na mbuzi kwa jamii ili waweze kupata mbolea, lishe na kipato katika kaya
- AFYA
Shirika linatoa elimu ya lishe kwa jamii kwa kutoa mbegu za mboga mboga na matunda,pia linatoa elimu ya magonjwa mbali mbali ikiwemo Maralia, UKIMWI na Virusi vya UKIMWI kwa jamii pia kusambaza vifaa kinga.
- UJASILIAMALI
Shirika linatoa elimu juu ya uibuaji/utambuzi
wa fursa katika maeneo jamii iliko, uanzishaji wa miradi ya
uzalishaji kama vile ufugaji wa Samaki, kuku, Nyuki, Mbuzi, Bustani za boga
boga na matunda na Uuzaji wa miche ya
miti. Pia shirika linawezesha uundaji na uendelezaji wa vikundi vinavyojishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo uzalishaji na masoko, kuweka na kukopa kwa kutoa elimu na vifaa.