Kuhusu FLCAD

USAJILI WETU.
Foundation for Local Capacity in Agricultural Development (FLCAD) ni shirika lisilo kuwa la kiserikali (NGO) lililosajiliwa chini ya sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikari Na.24/2002 iliyorekebishwa  mwaka 2005, kwa usajili namba OONGO/08231 mwezi Octoba 2015.

DIRA YA YETU
Kuwa na jamii yenye afya na kipato.
 
DHAMIRA YA YETU.
Kuchangia kujengea uwezo wa makundi maalumu katika jamii ili waweze kushiriki katika shughuli za maendeleo na hatimaye waishi maisha bora. 

MALENGO YETU.
  • Kukuza uelewa  kwa jamii juu ya kuongeza kipato, uhifadhi mazingira, kilimo na ufugaji wenye tija. 
  • Kuwezesha shirika kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali, sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kwa kuwa na mikakati ya pamoja katika maeneo yenye maslahi kwa pamoja ili kuwepo na maendeleo endelevu.
  • Kuwezesha mabadiliko ya sheria na sera zinazohusu kilimo, ufugaji na mazingira ili ziwe zenye tija.
  • Kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika mipango ya maendeleo.
MAADILI YETU
  • Uwazi na ukweli
  • Uwajibikaji.
  • Usawa wa ki-jinsia. 
  • Ushirikishaji.
  • Kujitolea.
  • Uhuru.
  • Uaminifu
  • Uadilifu
ENEO LA KAZI NA WANACHAMA WA SHIRIKA.
Shirika la FLCAD  limesajiliwa kufanya kazi Tanzania bara kwa sasa linafanya kazi katika wilaya ya kyerwa, Mkoani Kagera nchini Tanzania  likiwa na wanachama  68 ( wanawake 32, wanaume 36).
 
WALENGWA.
Ni jamii ya watu wanaoishi vijijini hasa wanawake, vijana na watoto.

WANUFAIKA WA HUDUMA ZITOLEWAZO NA FLCAD.
Idadi ya walionufaika moja kwa moja ni watu 6,356 (Wanawake 2,473, wanaume 2,215,Vijana 914, na watu wenye mahitaji maalum 754) 









Where tree grow people grow

 

FLCAD DOCUMENTS